Tuesday, December 10, 2013

AIRTEL YAMWAGA ZAWADI YA MILIONI 40 KATIKA 'MIMI NI BINGWA' PROMOSHENI

Displaying Mbagala 7.jpg 
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, (Kushoto) akiwaonyesha wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam –Rashid Ahmed Othman (wa pili kushoto) na Peter Elias Magusha (wa tatu kushoto), jinsi mashine inavyochangua namba ya mshindi katika droo ya Mimi ni Bingwa promotion iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki Mbagala Zakiem na kutangazwa washindi watano wa wiki hii wa shilingi milioni moja moja. Zaidi ya shilingi milioni 40 tayari zimetumwa kwa washindi mbali mbali na tiketi nne kwa washindi wawili wa wiki kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford. Kulia ni Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.

KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzani imeshazawadia wateja wake zaidi ya shilingi milioni 40 katika promosheni yake ya 'Mimi ni Bingwa' yenye lengo la kuwazawadia wateja wake na kuongeza chachu ya mpira wa miguu nchini.

Hii ilithibitishwa na Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando wakati wa kuangalia mechi ya Ligi kuu ya Uingereza kati ya klabu ya Manchester United na Newcastle iliyoonyeshwa bure eneo la Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam.
Alisema mbali na zawadi ya fedha inayotolewa kwa kutumwa kupitia Airtel Money, washindi wawili wa tiketi pamoja na safari inayogharamiwa na Airtel kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live) za klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford, watasaidiwa katika utafutaji wa hati za kusafiria pamoja na washindi wawili watakaopatikana katika droo ya wiki ya tatu na nne.

Mmbando ambae wakati wa tukio pia alitangaza washindi wengine watano wa shilingi milioni moja kila mmoja wa wiki hii, alisema promosheni inayotokana na ushirikiano kati ya Manchester United na kampuni hiyo ya simu hailengi tu kuwazawadia wateja lakini pia kuwaunganisha wateja na soka la kimataifa hatua ambayo itaongeza chachu ya wapenda michezo Tanzania.

''Airtel imeweka vituo mbali mbali ambavyo wapenda soka wataangalia mechi za klabu ya Manchester United bure kupitia luninga kubwa. Leo tunawaonyesha wakazi wa Mbagala mechi kati ya Manchester United na Newcastle, lakini pia tunavituo vingine ambavyo tunaonyesha mechi zote za Man U bure. Vituo hivi ni kama Mbeya, Shaba Pub Mwanza -Shooters Pub, Dodoma - Four Ways, Dar es Salaam - Rose Garden, Morogoro - Nyumbani Launge na Arusha - Empire Sports bar,'' alisema Mmbando.

Mmbando alisema kuwa bado zawadi nyingi kushindaniwa na kusema kuwa mbali na shilingi milioni 2 za kila siku, milioni 10 kila wiki na tiketi 2 kwa watu wawili kila wiki, bado kuna zawadi ya kubwa ya shilingi milioni 50 kushindaniwa mwishoni mwa promosheni.
Alisema ili mteja kushiriki kwenye promosheni, anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) yenye neno "BINGWA" kwenda namba 15656.

Licha ya washabiki wa Man U kuvunjika moyo baada ya kufungwa goli moja na Klabu ya Newcastle United katika mechi iliyochezwa uwanja wa Old Trafford  waliburudishwa na wasanii wa Bongo Flava kama Ney wa Mitego, Young Killer na Kinoko Comedy Group.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU