Meneja wa Bia ya Ndovu special malt Pamela kikuli
kushoto akimkabidhi mwakilishi wa asasi ya Palms Foundation Maximilan Jones
kulia mfano wa hundi ya kiasi cha
shilingi milioni kumi kwaajili ya kusaidia kununulia vifaa vya kufanikisha
kampeni ya kuwalinda wanyama aina ya Tembo hapa nchini,Katikati ni Meneja
mahusiano na mawasiliano wa tbl Editha Mushi.
Mwakilishi wa asasi ya Palms Foundation Bwana Maximilan
Jenes kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkakati wa matumizi ya
shilingi milioni kumi walizopatiwa na Kinywaji cha Ndovu Special Malt juu ya
kueneza elimu ya kuwalinda wanyama Tembo nchini, Katikakati ni meneja mahusiano
na mawasiliano wa Tbl Editha Mushin a kushoto ni meneja wa ndovu special malt
Pamela Kikuli.
Meneja wa Bia ya ndovu Special Malt Pamela Kikuli kulia
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya kampeniu ya kueneza habari na
elimu juu ya kuwalinda wanyama Tembo nchini, kulia ni Meneja mahusiano na
habari wa tbl Edith mushi.
BIA ya Ndovu imetoa kiasi cha Sh milioni 10
kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kuwalinda tembo, wanyama ambao wanazidi
kutoweka kutokana na kuuliwa kila siku kwa ujangili.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo
jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli alisema, fedha
hizo zimepatikana kutokana na kampeni kubwa iliyokuwa ikiendeshwa kwa
kushirikisha Watanzania, katika kueneza habari za umuhimu wa uhifadhi wa tembo.
“Bia ya Ndovu ilianza ushirikiano na asasi ya
Pams Foundation kwa lengo la kuelimisha na kuisaidia jamii katika juhudi za
kulinda wanyama, hasa tembo ambao karibu kila siku wanauawa 30 kwa njia ya
ujangili.
“Zoezi hili la kukusanya fedha na kuwaelimisha
Watanzania kwa ujumla tumelifanikisha na leo hii tunakabidhi kiwango hiki cha
fedha taslimu kwa Pams Foundation. Ni tumaini letu kuwa fedha hizi zitatumika
kama zilivyokusudiwa kwa ajili ya faida ya kutoa elimu na kununua vifaa vya
kusaidia kuwalinda wanyama hao,” alisema Pamela.
Akipokea msaada huo, mwakilishi wa
mfuko huo, Maximillan Jenes alisema, fedha hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa
kuhakikisha ujumbe na elimu juu ya kulinda wanyama hao unawafikia wengi, ikiwa
pia kununua vifaa mbalimbali vya kwa askari wanyamapori wanaopambana kuwalinda.
“Watanzania pia tunapaswa kubadilika na kuweka mikakati ya kuwalinda tembo
waliobaki hapa nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, pia
tunawashukuru Ndovu kwa msaada wao huu,” alisema.
Naye Meneja Uhusiano na
Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi alisema, hiyo ni
sehemu ya kampeni za kampuni hiyo kuhakikisha inashirikiana na jamii katika
kuwalinda tembo.
“Bia ya Ndovu imefanikisha na
itaendelea kufanikisha kusambaza ujumbe kwa jamii juu ya uhifadhi wa tembo na
kuwapa Watanzania imani kubwa ya kuweza kukabiliana na changamoto hii.”
Bia ya Ndovu inazalishwa na
kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 maoni:
Post a Comment