Friday, December 27, 2013

KALAMA NYILAWILA KUMVAA IBRAHIMU MAOKOLA DESEMBA 31 MSASANI KLABU

Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza makaburini, Bernald Lumbila (kulia) akimwelekeza bondia Kalama Nyilawila jinsi ya kupiga ngumi katika mbavu. Nyilawila anajiandaa na mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu jijini Dar es salaam.
Kalama Nyilawila akijifua 
 
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ya kumkabili mpinzani wake Ibrahimu Maokola Desemba 31,mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha mabondia mbalimbali.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari,Kalama ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwani ana usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini

Mpambano huo utaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya mpambano wa kimataifa na mapambano mengine ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde uku Cosmas Cheka akioneshana ubabe na Iddy Mnyeke mpambano mwingine ni Antoni Mathias atakae menyana na Fadhili Majiha mapambano yote ya utangulizi ni ya raundi sita sita 

siku hiyo itasindikizwa na burudani za kila aina akiwemo mwana hip hop mashuhulu Kala Pina, Kimbunga Noma na wengine wengi ambao wata uanga mwaka na kukaribisha mwaka mpya kwa njia ya burudani

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU