Katibu
wa kamati ya maandalizi ya uhurumarathon Innocent Melleck akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya maandalizi na wasanii
watakaoshiriki kwenye mkesha wa Uhuru utakaofanyika viwanja vya Leaders
Club baada ya kukamilika kwa mbio za uhuru kushoto ni katibu mkuu wa
shirikisho la riadha Tanzania Selemani Nyambui
ZIKIWA zimebaki siku
chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kufanyika,
wasanii watakaotoa burudani siku ya mkesha wa uhuru wameapa kufanya kweli.
Wasanii wanaotarajiwa
kutoa burudani ni Roma Mkatoliki, Joh Makini, G Nako, Nick wa Pili, Mrisho
Mpoto, Mrisho Mpoto, TMK Wanaume, Mfalme Siboka na kundi la Twanga Pepeta.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti, wasanii hao walisema wanashukuru kupewa heshima kubwa kutumbuiza siku
hiyo na hasa ukichukulia umuhimu wa amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
“Nitafanya makamuzi ya
kweli siku hiyo na watu wategemee mistari iliyokwenda shule,” alisema Roma
Mkatoliki, huku Mrisho Mpoto akidai ana vitu vikali zaidi atakavyoweka
hadharani siku hiyo.
Naye Katibu wa Kamati ya
Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya mbio hizo imepanda, hasa
baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa mataifa mbalimbali.
Melleck alisema, mbali na
wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha
lengo la mbio hizo.
Alisema usajili bado
unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki
wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa
kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
0 maoni:
Post a Comment