Mkurugenzi
mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya
kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi
ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele
ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa
rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili
waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri
ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Askari
wa hifadhi ya mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamesimama
wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ambaye hayuko pichani wakati
akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika
chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali
za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
Askari wa hifadhi ya mbuga ya wanyama
(TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN
KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao
waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa
wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu
hao wafanye kazi kwa uaminifu.
Picha na Katavi yetu Blog
0 maoni:
Post a Comment