Monday, January 6, 2014

EUSEBIO KUZIKWA LEO HUKU MANCHESTER UNITED IKIAGA MASHINDANO YA FANguli wa soka wa URENO, EUSEBIO DA SILVA FEREIRA aliyefariki dunia hapo jana kwa maradhi ya moyo anatarajiwa kuzikwa hii leo katika mji wa Lisbon, ambapo kabla ya mazishi yake jeneza lake litatembezwa katika nyasi za dimba la LIGHT kama ambavyo yeye mwenyewe alisema kabla ya kifo chake.

EUSEBIO mzaliwa wa MSUMBIJI, alijulikana kama BLACK PANTHER yaani chui mweusi kutokana na umahiri wake dimbani.

Serikali ya URENO imetangaza siku tatu za maombolezo ya nguli huyo wa soka.

Timu ya Manchester united imeondolewa katika hatua ya tatu ya michuano ya kombe la FA baada ya kufungwa MABAO mawili KWA MOJA na SWANSEA CITY katika mchezo uliochezwa jana kwenye uwanja wa OLD TRAFFORD.

Mabao ya washindi ya SWANSEA CITY yalifumgwa na Wilfried Bony na Wayne Routledge wakati bao la kufutia machozi la UNITED limefungwa na  Javier Hernandez,CHICHARITO.

Nayo Chelsea imetinga hatua ya nne ya michuano hiyo baada ya kuichapa timu ya daraja la kwanza ya Derby County mabao mawili kwa bila, huku Liverpool nayo imetinga hatua hiyo kwa kuifunga OLDHAM ATHLETIC kwa magoli mawili kwa bila.

Matokeo mengine West Ham United imefungwa na timu ya daraja la pili ya Nottingham Forest magoli matano kwa bila huku Sunderland imeichapa timu ya daraja la tatu ya Carlisle United magoli mawili kwa moja.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU