Wednesday, January 15, 2014

RAMBIRAMBI MSIBA WA MWAMUZI MSEBULA


Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi Methusela Msebula kilichotokea juzi (Januari 13 mwaka huu) katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Mwamuzi Msebula ambaye alikuwa mwamuzi daraja la kwanza (class one) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, maradhi ambayo yalimsababisha kuwa nje ya uchezeshaji mechi za mpira wa miguu kwa karibu misimu miwili.

Msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani, Msebula alitoa mchango mkubwa katika fani ya uamuzi nchini, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima. Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo (Januari 15 mwaka huu) nyumbani kwao Kanyigo, Bukoba mkoani Kagera.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Msebula, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU