Saturday, January 11, 2014

SULTAN SIKILO AFARIKI DUNIA

Mweka Hazina wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa), Sultan Sikilo amefariki dunia na atazikwa leo katika makaburi ya Kibada, Kigamboni katika Manispaa ya Temeke.
 
Msiba huo umetokea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa amelazwa, akitokea hospitali ya Temeke ambako nako alilazwa kwa muda mfupi.
 
Ikumbukwe kuwa marehemu alichaguliwa miaka mitatu iliyopita na enzi za uhai wake alipitia nafasi mbali mbali katika chama ikiwa pamoja na ujumbe. Marehemu pia alikuwa Mweka Hazina wa Timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC).
 
Kutokana na msiba huu, tunawaomba waandishi wa habari za michezo nchini, wadau na jamii kwa ujumla kuwa karibu na familia yake katika kipindi hiki kigumu.
 
Mungu Ailaze Roho  ya Marehemu Sultani Sikilo Peponi, Amina.
Majuto Omary
Mwenyekiti Taswa SC
Kwa niaba ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa).

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU