WAZIRI wa mambo ya nchi za nje, BERNAD
MEMBE amethibitisha kuwepo kwa mpango wa kuwapeleka wanamichezo watakaoshiriki
mashindano ya JUMUIYA YA MADOLA baadae mwaka huu.
Waziri MEMBE ameyasema hayo wakati
alipokutana na waandishi wa habari kuelezea masuala mbalimbali likiwemo suala
la kuwanoa wanamichezo hao kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Jana katibu wa shirikisho la mchezo wa
riadha, SELEMAN NYAMBUI aliambia TBC kuwa wanamichezo hao watakwenda katika
nchi za UTURUKI, AFRIKA KUSINI na ETHIOPIA.
0 maoni:
Post a Comment