Friday, March 14, 2014

KUTANA NA DOREEN PETER NONI MJASIRIAMALI NA MBUNIFU WA MAVAZI NCHINI

MOblog Tanzania hivi karibuni ilifanya mahojiano na Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini Doreen Noni aliyehudhuria mkutano wa Uchumi Duniani uliofanyika huko Davos, Uswisi (World Economic Forum) mwezi uliopita juu ya yote anazungumzia nafasi ya Wanawake, Vijana na Ujasiriamali endelea…….
Doreen-Noni-at-Davos
MOblog: Ulipata nafasi ya kuhudhuria mkutano wa Uchumi duniani (World Economic Forum 2014) hebu tueleze ulipata vipi nafasi ya kuhudhuria?
Doreen: Mimi nilipata nafasi ya kuhudhuria (World Economic Forum) kupitia asasi ya Global Shapers ambayo ni delegation ya vijana kupitia World Economic Forum na vijana kuanzia miaka 20 mpaka 30 ambao kazi yao kuu ni kuangalia vijana ambao wanaleta mabadiliko katika jamii na ushiriki wa vijana katika maeneo mbalimbali, ya ujasiriamali kwa hiyo nilituma maombi kwenye jukwaa la Uchumi Duniani na wao wakaona nafaa kuhudhuria na nikahudhuria kwa hiyo nikawa mjumbe wa World Economic Forum kama kijana na jukwaa la kuwakilisha vijana wa bara la Afrika na nimehudhuria mikutano mitatu ya uchumi duniani mpaka sasa.
Doreen-Noni-Conference
Doreen: Nilikuwa kwenye session tofauti nilikuwa kwenye panelist mbalimbali, kama vile Innovation and Design na panelist nyingine ilikuwa Africa the next billionaire ambayo kulikuwa na marais mbalimbali kama vile Goodluck Ebele Jonathan; Rais wa Nigeria, Aliko Dangote; Afisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Group na John Mahama; Rais wa Ghana, hii session ilikuwa inaogelea kuhusu umati wa watu Afrika na vijana tulikuwa kama 50 ambao tulihudhuria mkutano huu na vijana wengi Afrika wanatuma maombi duniani na kila session wanataka vijana wahudhurie kwa hiyo wanataka kujua uwezo wa vijana katika maswala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kijamii.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU