Wednesday, March 26, 2014

WAJERUMANI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI

DSC_0080
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.(Picha na Zainul Mzige).
Na Damas Makangale, MOblog
HUKU Tembo wakiendelea kuuawa katika mbuga kadhaa nchini, Serikali ya Ujerumani imeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kupambana tatizo la ujangili Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe amesema serikali ya ujerumani imeahidi kutoa msaada wa vifaa na ujuzi wa kupambana na ujangili katik mbuga za Tanzania.
“tupo katika hatua za mwisho za ushirikiano wa kupambana ujangili na majangili ili kunusuru Tembo wetu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,” amesema Membe.
Waziri Membe amesema kwamba serikali ya Ujerumani imetoa magari ya kupambana ujangili, camera, vifaa vya kisasa na mafunzo kwa askari wa wanyamapori ili kuwajengea uwezo wa kupambana na majangili nchini.
DSC_0048
Picha juu na chini ni Baadhi ya wageni waalikwa na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani nchini.
Amesema tatizo la ujangili si la Tanzania peke yake linahitaji ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika na ulaya kwa sababu pembe za ndovu kuuzwa kwenye nchi hizo au kuwa kama njia ya kupitishia.
“wanatoa mafunzo ya kutosha kwa askari wetu wa wanyamapori ili waweze kukabiliana kikamilifu na majangili,” aliongeza
Waziri Membe alizungumza kwenye mkutano wa pamoja na Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani Dkt Frank-Walter Steinmeier ambaye alitembelea nchini kwa mara ya kwanza tangu kushika nyadhifa hiyo
Kwa taarifa ambazo zipo ni kwamba Tembo 25,000 waliuawa mwaka 2011 na 22,000 waliuawa mwaka 2012, ni ishara inayoonyesha kuwa biashara haramu ya wanyama pori sasa imekuwa ni uhalifu wa kidunia wenye nguvu ya kuathiri maendeleo ya kiuchumi, kusababisha migogoro, kuimarisha vikundi vya kigaidi na kuathiri watu wenye hali duni ya watu waishio katika umaskini.
Faru wanauawa na maharamia kila baada ya dakika 10 na ni wachache kuliko chui 3,500 ambao wamebaki porini.
Ujangili unaathiri jamii barani Afrika, hususan yale maeneo katika bara ambapo wanakabiliwa na hali mbaya ya janga la ujangili.
DSC_0054
DSC_0045
Sehemu ya waandishi wa habari nchini pamoja na waandishi kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo jijini Dar.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU