Tuesday, January 25, 2011

KUZIONA YANGA NA DEDEBIT YA ETHIOPIA NI SHILINGI ELFU 20

                                                                                    
 
Msemaji wa YANGA LOUIS SENDEU.
Timu ya YANGA inashuka dimbani kucheza na timu ya DEDEBIT ya ETHIOPIA katika mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho mchezo utakaofanyika katika uwanja wa TAIFA Jijini DSM.

Msemaji wa YANGA LOUIS SENDEU amesema timu hiyo inawasili Jijini DSM alhamsi wiki hii ikiwa na kikosi kizima ambacho kina wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje

SENDEU amesema klabu ya YANGA imepanga kuhamia kwenye kambi nyingine tofauti na kambi ya JANGWANI ambayo imezoeleka na wachezaji.

Waamuzi wa nchezo huo wanatoka nchini SUNDAN ambao nao wanatarajia kuwasili hapa nchini siku ya alhamis.

Katika hatua nyingine msemaji huyo ametaja viingilio kuwa ni shilingi elfu ishirini V.I.P, Elfu kumi ,Elfu tano na Elfu tatu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU