Wednesday, May 4, 2011

MASHINDANO YA POOL YA VYUO VIKUU KUANZA KATIKA MIKOA TOFAUTI

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya safari lager wanatangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya mchezo ya pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es asalaam Meneja wa bia ya safari Oscar Shelkindo amesema TBL kupitia Bia ya safari kwa mwaka huu imeongeza sehemu ya udhamini wake katikamchezo huo ambapo inaweza kuongeza mikoa ya vyuovikuu kutoka mmoja wa mwaka jana hadi kufikia mikoanane.

 Mashindano hayo mwaka jana yalishirikisha Dar es salaam pekee ambapo chuo kikuu cha Dar es salaam kilifanikiwa kuwa mabingwa wa mwaka jana. Kwa mwaka huu mashindano hayo yatahusisha mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha. Fainali zake zitafanyikia Mkoani Dodoma.

ZAWADI ZA MASHINDANO

Mwaka huu katika ngazi ya mkoa na kitaifa jumla ya shilingi milioni kumi na nane na laki sita zitatumika katika zawadi ya mkoa mshindi wa kwanza anapata laki tano, msindi wa pili atapata laki tatu na mshindi wa tatu laki mbili na mshindi wa nne elfu hamsini.

Katika mchezaji mmoja mmoja mshindi wa kwanza atapata laki moja na msshindi wa pili elfu hamsini. Ngazi ya taifa mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni mbili, mshindi wa pili atapata milioni moja na laki tano, mshindi wa tatu atapata milioni moja na laki tatu, mshindi wa nne atapata milioni  moja na mshindi wa tano hadi wa nane watapata kifuta jasho cha shilingi laki tano kila chuo.Ambapo upande wa mchezaji  mmoja mmoja mshindi atapata laki tatu na wapili laki mbili, mshindi wa tatu laki na nusu na mshindi wa nne laki moja

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU