TAIFA STARS v BAFANA BAFANA
Timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ inatarajia kuwasili nchini Mei 12
mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania
‘Taifa Stars’ itakayofanyika Mei 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nyota wote wa kikosi cha kwanza cha Bafana Bafana kinachofundishwa na PitsoMosimane wanatarajiwa kuwepo kwenye mechi hiyo, isipokuwa kiungo Steven Pienaar anayechezea timu ya Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.Bafana Bafana na Stars zote zina mechi ngumu ugenini za mchujo kusaka tiketi zafainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani EquatorialGuinea na Gabon. Stars itacheza Juni 4 mwaka huu jijini Bangui dhidi ya Jamhuriya Afrika ya Kati wakati Bafana Bafana itakuwa jijini Cairo, Juni 3 dhidi yawenyeji Misri.Stars itaingia kambini Mei 7 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya, Henry Joseph (Kongsvinger IL,Norway), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam),Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF,Sweden) wameshaombewa ruhusa katika klabu zao ili wajiunge na Stars kwa ajili yamechi hiyo.
MAPATO U23 TANZANIA v UGANDA (THE KOBS)
Pambano la mchujo la All Africa Games kati ya Tanzania U23 na Uganda U23 (TheKobs) lililochezwa Aprili 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingizash. 32,982,000 kutokana na watazamaji 24,078 walionunua tiketi.Watazamaji 22,117walilipa sh. 1,000, 1,749 (sh. 5,000) na 212 (sh. 10,000).
Baada ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,031,152.54 na gharamaza awali za mchezo sh. 16,950,000 mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; uwanja sh.1,100,084.75, gharama za mchezo sh. 1,100,084.75, Shirikisho la Mpira wa MiguuAfrika (CAF) sh. 550,042.37 wakati TFF sh. 8,250,635.59. Chama cha Mpira waMiguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata asilimia tano ya mgawo wa TFF ambayoni sh. 412,531.78.
Mwenyekit iKamati ya UchaguziVilla Squad Football ClubDAR ES SALAAM
YAH: UCHAGUZI WA VIONGOZI WA VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB
Rejea barua ya TFF yenye Kumbukumbu Na. TFF/ADM/EC.11/09 ya tarehe 30 Aprili2011 kuhusu somo hilo hapo juu iliyotimwa kwa Katibu wa Villa Squad FootballClub.
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Villa Squad kuzingatia Kanuni za Uchaguzi zawanachama wa TFF katika mchakato wa uchaguzi uliotajwa hapo juu.Ili kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi, Kamatiya Uchaguzi ya Villa Squad inakumbushwa kuzingatia viwango vya ada ya fomu zakuomba uongozi na pia tunaambatanisha ratiba ya mfano inayokidhi matakwa yaKanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF kwa urahisi wa rejea na kwa utekelezajiwa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Villa Squad.Wako katika michezo,
RATIBA YA UCHAGUZI WA VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB
Na. TAREHE SHUGHULI
1. 02/05/2011 Kamati ya Uchaguzi ya VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB (VILLA) kutangazaUchaguzi wa VILLA na nafasi za kugombea.03/05/2011 – 08/05/2011
Kuchukua fomu za kugombea uongozi VILLA. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe08/11/2011 saa 10:00 Alasiri.
Kamati ya Uchaguzi kupitia fomu za waombaji uongozi VILLA.Kutangaza matokeo ya upitiaji fomu na kuweka wazi kwenye mbao za matangazomajina ya waombaji uongozi VILLA 12/05/2011- 16/05/2011 Kutoa fursa ya pingamizi (kama zipo) kwa waombajiUongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 16/05/2011 saa 10:00 Alasiri
18-20/05/2011 Usaili na kutangaza matokeo /Kuwajulisha wagombea matokeo yausaili.7. 21 – 22/05/2011 Kutoa fursa ya kukata Rufaa, kwenye Kamati ya Uchaguzi yaTFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 22/05/2011 saa 10:00 Alasiri.
23-27/05/2011
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kusikiliza rufaa (kama zipo) na kutangaza matokeo yarufaa. (Kama hakuna rufaa, Kamati ya uchaguzi ya VILLA kutangaza majina yawagombea na nafasi zao na kuanza kwa Kampeni.
Baada ya uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya VILLAkutangaza majina ya wagombea na nafasi zao na kuanza Kampeni.
0 maoni:
Post a Comment