TUPO HAPA SAUDI ARABIA KIMALENGO KAMA KUFANYA KAZI, KUISHI, KUTEMBEA NA KADHALIKA. YOTE HAYO TUNATAKA AU TUNAPENDA NCHI YETU TANZANIA ITAMBULIKE NCHI ZA KIARABU NA DUNIANI KOTE.TUMEFANYA JUHUDI ZETU KUBWA SANA KUITANGAZA NCHI YETU TANZANIA NA IMETAMBULIKA KWA KIASI KIKUBWA SANA.
TULIFURAHISHWA SANA NA ZIYARA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, MHESHIMIWA MAMA SALMA KIKWETE, WAHESHIMIWA MAWAZIRI PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI YETU YA TANZANIA ILIYOFANYIKA MAPEMA TAREHE 14 APRIL, 2009 HADI TAREHE 17 APRIL 2009.KATIKA KIPINDI HICHO KIFUPI CHA SIKU TATU, MAAJABU YA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE NA UJUMBE WAKE YALIKUWA NI YA KUSISIMUA SANA. PICHA NA JINA LA TANZANIA LILIVUMA NA KUENEA KATIKA NCHI SOTE ZA KIARABU NA DUNIANI KOTE TUKATAMBULIKA, TUKATUKUZWA, TUKAPENDWA NA NA MENGI MENGINEYO YALIJITOKEZA AMBAYO NI MAZURI KWA TAIFA LETU CHANGA LA TANZANIA.
MHESHIMIWA RAIS KIKWETE ALITEMBELEA SEHEMU NYINGI SANA HAPA SAUDI ARABIA KAMA RIYADH CHAMBER OF COMMERCE AND INDUSTRY AMBAPO ALIKKUTANA NA WAFANYA BIASHARA WA KIMATAIFA, ALIKUTANA PIA NA HRH PRINCE ALWALEED BIN TALAL BIN ABDUL AZIZ AL SAUDI, CHAIRMAN OF THE KINGDOM HOLDING COMPANY, NA SEHEMU NYINGI KUZIORODHESHA ZOTE SIO RAHISI. HIVYO ALIPATA MENGI SANA YA KUVUTIA NA KUISAIDIA TANZANIA NA KUWAVUTA WAWEKEZAJI PIA WAFANYA BIASHARA WAKIMATAIFA.
MWISHO MAAJABU YA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE, MHESHIMIWA MAMA KIKWETE, WAHESHIMIWA MAWAZIRI NA VIONGOZI WOTE WALIMALIZIA ZIARA YAO HAPA SAUDI ARABIA KWA KUKUTANA NA JUMUIYA YA WATANZANIA WALIYOKO SAUDI ARABIA. KWA KWELI WATANZANIA ILIKUWA NI FURAHA KUBWA SANA AMBAYO HAITOSAHAULIKA TENA TUNAJIVUNIA SANA KWA MHESHIMIWA RAIS KWA JUHUDI ZAKE ZA PAMOJA ANAZOZIFANYA KULETA MAENDELEO KATIKA NCHI YETU KWA MANENO NA VITENDO.
SASA TURUDI KATIKA KILIO CHETU. BAADA YA ZIARA HIYO YA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE MATOKEO NA MAFANIKIO MAKUBWA SANA YALIPATIKANA.VIONGOZI WA MAKAMPUNI MBALIMBALI,WAFANYA BIASHARA, WAWEKEZAJI NA WATALII WALIMIMINIKA TANZANIA KWA SHANGWE FURAHA NA HAMU KUBWA KUPITIA OFISI YETU YA UBALOZI HAPA RIYADH SAUDI ARABIA WALIPOKELEWA NA KUSAIDIWA VIZURI SANA NA MAOFISA PAMOJA NA WAFANYAKAZI KWA BIDII NA MOYO WAO WOTE HAPA UBALOZI WA TANZANIA KWA HAKIKA KAZI ZAO ZINASIFIKA KWA UZURI. KIPINDI HICHO HAPAKUWA NA BALOZI MTEULIWA.
TATIZO KUBWA AMBALO LIMEWASHA MOTO MKALI NA KUPATA HASIRA KATIKA NYOYO ZETU NI KUPOTEA MAZURI NA SIFA ALIZOZIACHA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA YAKE HAPA SAUDI ARABIA NA JUHUDI ZETU ZA KUWAKARIBISHA WAGENI NYUMBANI TANZANIA. HII NI KWA SABABU YA UTAWALA MPYA ULIOLETWA NA BALOZI MPYA HAPA RIYADH SAUDI ARABIA.
WAGENI NA WAFANYA BIASHARA WAMEKATA SAFARI ZAO GHAFLA BAADA TU YA KUWASILI BALOZI MPYA HAPA RIYADH SAUDI ARABIA.KWAKUWA NI MTU ASIYETAKA KUONANA NA WATU.SISI WATANZANIA TUNAHASIRA SANA KWANI YAELEKEA KUWA BALOZI HUYU HAWEZI MAJUKUMU AU HAJUI AU AMESAHAU TUNAOMBA TUSAIDIWE MAWAZO.
NI MUDA WA MWAKA SASA TANGU BALOZI KUWASILI HAPA SAUDI ARABIA. MOJA YA MAAJABU ALIYOYAFANYA BALOZI HUYU NI KUKATAA KUONANA NA WATANZANIA WALIOKO HAPA SAUDI ARABIA HADI HII LEO. WANAJUMUIYA WALIJITOLEA MICHANGO MIKUBWA SANA KWA HALI NA MALI KUANDAA CHAKULA NA MAKARIBISHO YA KUJITATAMBULISHA NA KUMJUWA BALOZI MTEULIWA MARA MBILI KWA WAKATI TOFAUTI.KATIKA OFISI YA UBALOZI LAKINI PAMOJA NA YOTE HAYO ALIKATAA MWITO WETU WA KUKUTANA NA WATANZANIA. HIVYO TULIKUTANA NA MAOFISA WA UBALOZI LAKINI BALOZI MWENYEWE HAKUONEKANA JE KWELI TUTAFIKA HUKO TWENDAKO?
MHESHIMIWA RAIS KIKWETE ALITUONA JAPO ALIKUWA NA SIKU TATU TU. JE MHESHIWA BALOZI LEO AMEMALIZA MWAKA ATATUONA TENA? HATA HIVYO HATUNA HAJA YA KUMUONA NA WALA HATUMUHITAJI HAPA SAUDI ARABI TUNATAKA KWENDA MBELE SIO KURUDI NYUMA.
MVUTO WA NCHI YETU TANZANIA ULIVUMA SANA KABLA YA MWAKA LAKINI HIVI LEO UMEKWISHA ZIMIA KABLA HAUJAFA KABISA TUNAOMBA JUHUDI ZA HARAKA ZICHUKULIWE ILI KUOKOA MVUTO HUO.
WATANZANIA SAUDI ARABIA.
0 maoni:
Post a Comment