Wednesday, February 27, 2013

BABA MTAKATIFU BENEDIKTI XVI AKUTANA KWA MARA YA MWISHO NA WAUMINI ST. PETER'S SQUARE


                                                    Umati Mkubwa wa Waumini
                 Moja la jukwaa kubwa la wapiga picha wa kimataifa
     Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome alikuwepo kuiwakilisha Tanzania.
                Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma walikuwepo pia.
                       Baba Mtakatifu akiingia kwenye St. Peter's Square
                 Picha ya Baba Mtakatifu alipotupitia Karibu huku akitubariki
Bendera ya Tanzania

Baba Mtakatifu Benedikti XVI  tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku. 

Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.

Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.

Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU