Friday, November 26, 2010

AZAM YAIONYA YANGA KUKAA MBALI NA MCHEZAJI NGASA NA NCHUNGA AONYWA KUZUNGUMZIA JUU YA KUMHAMISHA NGASSA


KLABU ya AZAM FC imepinga kauli ya mwenyekiti wa YANGA, LLOYD NCHUNGA kwamba wamefanya mazungumza na wanataka kumrudisha katika timu ya YANGA, mshmabuliaji wa MRISHO NGASSA.

Mwenyekiti wa klabu ya AZAM FC, SAID MUHAMMAD ABEID amesema wanashangazwa na kauli ya mwenyekiti wa YANGA na kubainisha kuwa wana nia ya kumrudishia NGASSA katika klabu hiyo , bali YANGA wanania ya kumuathiri  kisaikoloji mchezaji wao ili asicheze vizuri soka lake katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo kama alivyoanza vibaya mzunguko wa kwanza

Aidha ABEID ameitaka klabu ya YANGA kufuata taratibu zinazotakiwa katika sheria za shirikisho la soka Tanzania TFF na lile la duniani FIFA kama wao walivyofanya wakati walipokuwa wakimuhitaji mchezaji Mrisho Ngassa akiwa mchezaji wa YANGA.

Mwenyekiti amesema hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa na YANGA na timu ya AZAM zaidi YANGA walipeleka maomba ya kumtaka NGASSA kwa mkopo katika mzunguko wa pili wa ligi jambo ambalo timu ya AZAM haiko tayari. 

Amesema klabu ya AZAM ipo tayari kukaa na YANGA na kukubaliana kiasi cha fedha ili mchezaji huyo aweze kurudi YANGA,lakini kipindi cha uhamisho wa dirisha dogo unamalizika kesho hivyo AZAM hauko tayari kukaa na YANGA kwa kipindi hiki kwani muda umeisha.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU