Mabondia CHARLES ANGAI na EMANUEL SHIJA wanatarajia kupanda ulingoni katika mchezo mpya wa ngumi ambazo watu hupiana kwa kutumia mwili mzima.
Mratibu wa mpambano huo JAPEHT KASEBA na mabondia hao wamesema kuwa mpambano huo utakuwa wa aina yake kwani ni mara ya kwanza kufanyika nchini ambapo kila mmoja wao amejigamba kufanya vyema.
KASEBA amesema kuwa mchezo huo ni mpya ambao wanaamini kuwa watanzania wengi wataupenda , ambapo ni tofauti na kutumia mateke na ngumi wa kickboxing.
Katika hatua nyingine ,KASEBA amesema kuwa mashindano ya ligi ya mabingwa AFRIKA kwa mchezo wa KICK BOXING itafanyika hapo mwakani ambapo mabondia mbali mbali watashiriki ambapo yatafanyikia hapa nchini.
0 maoni:
Post a Comment