mkurugenzi wa kampeni hiyo DAVID KYNE .
Wakati mashindano ya CECAFA TUSKER CHALENJI ikitarajiwa kuanza kesho , rais wa baraza la michezo kwa nchi za afrika mashariki na kati CECAFA , LEODGAR TENGA ametangaza nia ya kuwania kiti cha ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka kwa afrika CAF.
Nia ya TENGA kuwania kiti hicho imetangazwa leo na afisa wa habari wa CECAFA, FINNY MUYESHI wakati alipokutana na waandishi wa habari kuelezea masuala mbalimbali ya mashindano hayo na uchaguzi wa CAF uliopangwa kufanyika nchini SUDAN mwezi februari mwakani
Kuhusiana na mashindano ya CECAFA yanayoanza jumamosi hii, MUYESHI amesema michezo yote itachezwa katika uwanja wa TAIFA na viwanja vingine viwili vya UHURU na KARUME vitatumika kwa mazoezi.
Mbali na mashindano hayo pia, waratibu wa kampeni ya malaria haikubaliki kupitia mkurugenzi wa kampeni hiyo DAVID KYNE amesema wanatumia fursa ya mashindano hayo kuzidi kuhamasisha mashabiki wa soka kuhusiana na nia ya kupunguza malaria usienee
Naye kamanda wa polisi kanda maalum ya DSM, SULEIMAN KOVA amesema jeshi lake limejipanga katika suala la ulinzi na usalama
Michezo ya ufunguzi jumamosi hii ni kati ya KILIMANJARO STARS na ZAMBIA na mchezo mwingine ni kati ya BURUNDI na SOMALIA.
0 maoni:
Post a Comment