MABINGWA WA TAIFA POOL KINONDONI.
Chama cha mchezo wa POOL wilaya ya KINONDONI kimeandaa sherehe maalum kwa ajili ya kuianga timu ya TAIFA ya POOL inayokwenda nchini UFARANSA kushiriki mashindano ya DUNIA pamoja na kuipongeza timu ya KINONDONI kwa kutwaa ubingwa wa TAIFA.
Akizungumza kwa njia ya SIMU mweka hazina wa pool KINONDONI ZAHORO amesema sherehe hii ni kuwatia moyo wachezaji kabla ya kwenda nchini UFARANSA pamoja kuwahamasisha wachezaji wa kinondoni kuzidi kujituma zaidi.
Timu ya TAIFA ya mchezo wa POOL inatarajia kuondoka nchini Jumamosi wiki hii ikiwa na wachezaji saba ambao wanakwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya DUNIA ya POOL yanatorajia kuanza kufanyika mapema mwezi huu
Pia KINONDONI ilitwaa ubingwa wa taifa baada ya kuifunga timu ya ILALA ambao walikuwa mabingwa mwaka jana , kwa upande wa wanawake ubingwa huo ulikwenda kwa mchezaji kutoka KINONDONI VIOLETY MREMA ambaye baada ya ubingwa huo amepata nafasi ya kwenda nchini UFARANSA kushiriki mashindano ya DUNIA.
0 maoni:
Post a Comment