Tuesday, November 16, 2010

MASHIRIKISHO YA SANAA YAJA NA MIKAKATI MIZITO YA KUWAKOMBOA WASANII

Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamale (Mwenye shati la mistari) naye alitaja mikakati ya shirikisho lake ambapo aliweka wazi mkakati wa kujenga Maktaba kubwa ya sanaa za ufundi (Art Gallery).
Jopo zima la marais wa mashirikisho kutoka kushoto ni Ibra Washokera (Muziki), Adrian Nyangamale (Ufundi), Agnes Lukanga (Maonyesho) na Symon Mwakifwamba (Filamu
 Rais wa Shirikisho la Filamu, Symon Mwakifwamba (Kulia) akionesha moja ya habari kwenye  gazeti iliyokuwa na taarifa za uvunjifu wa maadili za mmoja wa wasanii wa filamu.Aliahidi kupambana na hali hiyo katika tasnia ya filamu.

 
Mashirikisho ya Sanaa nchini yametaja mikakati ya kuikomboa tasnia ya sanaa dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mipango madhubuti inawekwa katika kuwafanya wasanii kuwa na maisha bora na kufanya kazi zenye ubora na zinazokubalika ndani na nje ya nchi.
 
Marais wa mashirikisho hayo ambao ni Symon Mwakifwamba (Filamu), Adrian Nyangamale (Ufundi), Ibra Washokera (Muziki) na Agnes Lukanga (Maonyesho) waliweka wazi mikakati hiyo wakati wakiwasilisha mada kwa pamoja (Panel Discussion) kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii katika Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
 
Baadhi ya mikakati iliyotajwa na marais hao ni ya kuhakikisha sheria ya hakimiliki na haki shiriki inaangaliwa upya, kupambana na maharamia wa kazi za wasanii, kujenga mtandao mpana wa mashirikiano baina ya wasanii,kuimarisha uongozi wa vyama mbalimbali vya wasanii, kupambana na unyonyaji dhidi ya wasanii na kujenga maktaba za sanaa (Art Galleries)  ambamo kazi mbali za sanaa zitahifadhiwa.
 
Rais wa Shirikisho la Filamu Symon Mwakifwamba yeye aliweka wazi kwamba, kazi kubwa waliyonayo ni kupambana na maharamia wa kazi zao, kuandaa tuzo za filamu (people’s choice awards) ambazo zinatazamiwa kufanyika Februari mwakani, uvunjifu wa maadili na tabia chafu za wasanii wa filamu ambazo katika siku za hivi karibuni zimekuwa zikilalamikiwa na wadau kiasi cha kuacha maswali mengi juu ya hatma ya wasanii wa tasnia hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU