Mkurugenzi wa hoteli ya PEACOCK DAMAS MFUGALE akizungumza ofisini kwake na waandishi wa TBC kuhusiana na usiku wa mtanzania ambapoamesema
wasaniii wa muziki wa dansi SIKINDE NGOMA YA UKAE pamoja na mwanamuziki LADY JAYDEE ni miongoni mwa wasaniii watakaopamba tamasha la burudani la mtanzania utakaofanyiia tarehe 3 mwezi ujao ambapo zaidi milioni thelathini zinatarajiwa kuchangishwa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima.
Mkurugenzi wa hoteli ya PEACOCK DAMAS MFUGALE ambao ndio wanaoandaa tamasha hilo, amesema kuwa lengo lao kurejesha faida kwa watanzani ambao ni wateja wao wakubwa
MFUGALE amesema kuwa mbali na burudani hizo pia kutakuwa na burudani ya nyimbo za asili za makabila mbali mbali ya watanzania pamoja na vyakula mbali mbali kutoka katika makabila hayo.
Katika hatua nyingine, MFUGALE amesema watarajia pia kufanya tamasha la burudani litakalo jumuisha nchi za AFRIKA MASHARIKI.
0 maoni:
Post a Comment