Kocha wa timu ya YANGA B KENNETH MKAPA.
Kocha wa timu ya YANGA ya vijana ya umri chini ya miaka 20 KENNETH MKAPA amesema kutoa sare kwa timu yake dhidi ya AFRIKA LYON ni uzembe wa washambuliaji wake ambao hawakuwa makani wakati wa umaliziaji.
Amesema mechi hiyo ilikuwa ya msingi kwao kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi katika mashindano ya UHAI CUP lakini pia amesema wanaendelea kujipanga zaidi ili kushinda mechi zinazofuata.
Katika mchezo huo timu ya YANGA imetoka sare ya bila kufunaga na timu ya AFRIKA LYON katika mashindano yanaoendelea katika uwanja wa KARUME JIJINI DSM
0 maoni:
Post a Comment