Msemaji wa TFF MICHAEL WAMBURA baada ya kuripoti ofisini.
Katibu Mkuu mpya wa shirikisho la soka hapa nchini TFF ANGETILE OSEAH pamoja na Afisa habari mpya wa shirikisho hilo BONIFACE WAMBURA wameripoti ofisini huku wakidai kuwa wataweka hadharani mikakati yao wiki ijayo mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jumatano wiki hii.
Katibu Mkuu huyo pamoja na Afisa habari wa TFF wamesema hayo wakati wakiripoti kwa mara ya kwanza katika ofisi za TFF zilizopo katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Watendaji hao wapya wa TFF ambao wameanza kazi rasmi hii leo kuziba pengo la Katibu Mkuu wa zamani Frederick Mwakalebela na aliyekuwa Afisa habari wa shirikisho
hilo Florian Kaijage.
0 maoni:
Post a Comment