Friday, January 14, 2011

STARS VS SUDANI SASA KUCHEZWA JUMAMOSI

  
Mechi kati ya timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS na SUDAN kuwania nafasi ya tano ya michuano ya kombe la MTO NILE iliyokuwa ichezwe leo imeahirishwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.

Habari kutoaka MISRI zinasema mechi hiyo imeahirishwa kutokana na mvua kunyesha.

Kumbuka mechi hii ilikuwa ya kufuta machozi kwa TAIFA STARS kwasababu ilikwishapoteza matumaini ya kusonga mbele kwenye nusu fainali baada ya kufungwa magoli SITA kwenye mechi mbili, na haikushinda mchezo hata mmoja zaidi ya sare ya goli MOJA kwa MOJA na UGANDA.

Kama TAIFA STARS itashinda mechi hii dhidi ya SUDAN itarejea hapa nyumbani na kitita cha shilingi MILIONI AROBAINI, ambazo si hapa ukilinganisha na MILIONI 30 za ubingwa wa CECAFA YAHEE
                                                         


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU