Monday, February 7, 2011

KUZIONA STARS NA PALESTINA KIINGILIO CHA CHINI ELFU MBILI NA JUU ELFU KUMI


Shirikisho la  soka nchini TFF limetangaza viingilio vya bei  ya chini vya  mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya TANZANIA TAIFA STARS dhidi ya timu ya taifa ya PALESTINA utakaofanyika jumatano wiki hii katika uwanja wa taifa huku kiiingilio cha bei ya chini kikiwa ni shilingi elfu moja na kikubwa kikiwa ni elfu kumi juu.
Ametaja viiingilio vingine kuwa ni elfu mbili, elfu tatu na elfu saba ambapo amewataka mashabiki wa soka kuhudhuria kwa wingi mchezo huo ili kuipa timu hamasa ya kufanya vyema.

Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi ODEN MBAGA,HAMIS MASWA,HAMIS CHANGWALU na RAMDAHANI KIBWA.

Katika hatua nyingine , WAMBURA amesema kuwa mtihani wa fifa wa  mawakala wa wauzaji wa wachezaji utafanyika tarehe 31 mwezi machi ambapo mawakala watakaofaulu mtihani huo wataweza kutambuliwa na fifa na kupata kibali.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU