Kikosi cha YANGA
Kocha wa YANGA, FRED FELIX MINZIRO amekiri kuwa wachezaji wake walifanya makosa ya kimchezo wakati timu yake ilipocheza na DEDEBITS na hivyo kusema kuwa makosa hayo ameyarekebisha na wachezaji wake wapo tayari kuikabili MTIBWA SUGAR katika mchezo wa ligi kuu soka TANZANIA BARA hapo kesho katika uwanja wa TAIFA.
MINZIRO amesema ijapokuwa kikosi hicho kipo tayari bado golikipa wa timu hiyo ambaye aliumia wakati wa mchezo dhidi ya DEDEBIT BERKO kama atakuwa fiti kucheza mchezo huo
Huku kocha huyo akifurahi kurudi kwa kiungo wake ATHUMAN IDD lakini hatocheza katika mchezo dhidi ya MTIBWA SUNGAR mpaka baada ya wiki mbili kupita.
Timu ya YANGA inashuka dimbani kucheza na MTIBWA SUGAR ikiwa na pointi 31 ikifuatiwa na SIMBA na AZAM FC.
Katika hatua nyingine mechi ya YANGA na KAGERA SUGAR iliyokuwa ifanyike FEBRUARI 5 mjini KAITABA umesogezwa mbele siku moja.
0 maoni:
Post a Comment