Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza mabadiliko ya baadhi ya mechi za ligi kuu TANZANIA BARA ili kutoleta mgongano wa mechi katika ligi hiyo.
Msemaji wa TFF BONIFACE WAMBURA amesema mchezo namba 85 kati ya AZAM na TOTO AFRIKA ya MWANZA uliopangwa kuchezwa Februari 4 katika uwanja wa UHURU sasa kufanyika FEBRUARI 5 .
Mchezo kati ya POLISI DODOMA dhidi ya SIMBA uliopangwa kufanyika Februari 5 umesogezwa mbele siku moja kupisha sherehe za maazimisho ya chama cha mapinduzi kitaifa zinafanyika mkoani DODOMA katika uwanja wa JAMHURI.
Na mchezo kati ya JKT RUVU na AFRIKA LYON ulipangwa kufanyika Februari 5 uwanja wa UHURU Jiji ni DSM umesogezwa mbele hadi Februari 7 mwaka huu.
Katika hatua nyingine semina ya makatibu wa wakuu ya vyama vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya michuona ya vijana ya COPA COCA COLA inatarajia kufanyika Februari 5 TEMEKE.
0 maoni:
Post a Comment