Thursday, February 10, 2011

TUZO YA MWANAMICHEZO BORA WA 2010 KUTOLEWA MEI 6 MWAKA HUU


Katibu mkuu wa cha chama waandishi wa habari za michezo AMRI MHANDO amesema tuzo ya mwanamichezo bora ya mwaka jana inatarajiwa kutolewa MEI 6 mwaka huu katika ukumbi wa WATERFRONT Jijini DSM.

Amesema bado wanaendelea na mazungumzo na makampuni mengine kupata udhamini wa kufanikisha utoaji tuzo hiyo.

Mwaka juzi  tuzo ya mwanamichezo bora ilikwenda kwa mcheza netiboli MWANAIDI HASSAN ambaye amechipukia katika mchezo wa netiboli na kuwazidi wachezaji wakongwe ,lakini pia tuzo ya mwaka huu imekuwa na utofauti mkubwa kutokana na TASWA kuambua kuwapa nafasi viongozi wa vyama vya michezo kuchagua wachezaji watatu kwa kila chama ambao watashindana katika kupata tuzo ya mwaka jana tofauti na ilivyokuwa ikifanyika miaka ya nyuma.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU