Mashindano ya Kombe la TAIFA yamezinduliwa leo jijini DSM na yataanza kutimua vumbi katika ngazi ya wilaya kuanzia tarehe 7 mwezi MAY huku wadhamini wakuu kampuni ya bia nchini TBL kupitia bia yake ya KILIMANJARO wakitumia milioni 800 kufanikisha mashindano.
Akizunguzma katika uzinduzi huo meneja wa bia ya KILIMANJARO GEORGE KAVISHE amesema kuwa kampuni yake imedhamiria kuinua vipaji vya wachezaji chipukizi ili kuinua kiwango cha soka la TANZANIA .
KAVISHE amesema kuwa bingwa wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha shilingi milioni arobaini, mshindi wa pili milioni ishirini huku mshindi wa tatu atazawadiwa milioni kumi.
Kwa upande wake , katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF ANGETILE OSIAH ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo ameshukuru kwa udhamini huo na kuwataka viongozi wa soka mikoani kusaka wadhamini watakaowasaidia katika maandalizi.
Kwa mujibu wa OSIAH mashindano hayo yataanza katika ngazi ya wilaya na baadae mkoa ambapo ametoa angalizo kuwa endapo mchezaji ambaye ahatapitia katika ngazi hiyo hatacheza katika michuano hiyo nagzi ya mkoa.
0 maoni:
Post a Comment