Bondia AWARDH TAMIM akiongea na waandishi wa habari pembeni akiwa na kocha wake JUMA SULEIMAN .
Bondia AWARDH TAMIM ametolea ufafanuzi suala la hali yake kufuatia kuzuka hali ya nsintofahamu juu ya afya ya bondia huyo baada ya kuonesha hali ya kuchanganyikiwa alipotangazwa mshindi wa pambano lake na ASHRAF SULEIMAN.
Kwa upande wake mwalimu wa bondia huyo JUMA SELEMANI amefurahishwa na kiwango alichoonesha bondia wake na kuahidi kuendelea ili kumnoa ili awanie ubingwa wa Afrika
AWARDH TAMIMU alifanikiwa kutetea ubingwa wake wa ngumi uzito wa juu wa AFRIKA MASHARIKI na KATI, kufuatia mpinzani wake ASHRAF SULEIMAN kushindwa kurejea ulingoni katika raundi ya saba.
0 maoni:
Post a Comment