Sunday, March 20, 2011

SHEREHE ZA KUCHANGIA ZANZIBAR HEROES KUFANYIKA MACHI 26 MWAKA HUU VISIWANI ZANZIBAR

Kampuni ya FUTURE CENTURY SPORTS LIMITED imeandaa sherehe za kuchangia timu ya TAIFA ya ZANZIBAR ili iweze kuwa fedha za kujiendesha katika michezo mbalimbali inapoandaliwa .

Mkurugenzi wa kampuni hiyo HEREN MSANJA amesema nia yao ni kukusanya US DOLA 200000 ili kuisaidia timu ya ZANZIBAR kufanikisha maendeleo ya soka kwa timu ya ZANZIBAR.

Sherehe hizo za kuchangia timu ya ZANZIBAR zitaongozwa na Rais Rais wa serikali ya Mapindunzi ZANZIBAR SHEIN na zimepangwa kufanyika Machi 26 mwaka huu huko visiwani ZANZIBAR,hivyo wadau mbalimbali wa soka wanaobwa kufika kuchangia timu hiyo ambayo haina kipato chochote katika kujiendeleza yenyewe kwa michezo ya ndani na ya nje ya nchi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU