Friday, March 4, 2011

TENGA ATETEA NAFASI ZAKE NDANI NA NJE YA NCHI

Rais wa TFF LEODGER TENGA kushoto na Msemaji wa TFF WAMBURA wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini DSM 

Rais wa shirikisho la soka la nchini TFF, LEODIGAR TENGA amekiri kuwa na jukumu zito la kuzitumikia nafasi za kazi  katika kuendeleza mchezo wa soka ndani na nje ya nchi  kutokana na kuwa na vyeo vingi

Kauli ya TENGA imekuja baada ya kushinda nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani AFRIKA CAF  huku akiwa Rais wa TFF mbali na nafasi hiyo pia TENGA anatarajiwa kuwania nafasi nyingine NOVEMBA mwaka huu , huku kiongozi huyo akiwa anashikilia nafasi ya Urais wa baraza la soka kwa nchi za Afrika mashariki na kati (CECAFA).

TENGA amesema nafasi aliyopata atatumia kuhakikisha asaidia kuleta maendeleo ya soka katika nchi za AFRIKA MASHARIKI

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU