Klabu ya YANGA kwa kupitia msemaji wake LOUIS SENDEU amesema uwanja wa KAUNDA pamoja na jengo la YANGA la mtaa wa MAFIA vinashindwa kufanyiwa marekebisho kutokana na kukosekana kwa hati za mali za hizo.
Msemaji amesema uongozi wa YANGA inahangaika kutafuta hati za uwanja pamoja na jengo hilo lakini mpaka sasa haijulikani hati hizo ziko wapi ili marekebisho yaanze kufanyika kama ilivyopangwa.
Amesema kwa mwanachama yoyote ambaye anajua hati hizo zilipo apeleke taarifa polisi ama klabuni yanga ili kazi iweze kufanyika kama kawaida .
KUHUSU MATAWI YA YANGA KUGOMBANA JUU YA MAKAMU MWENYEKITI.
Msemaji huyo amekanusha taarifa juu ya matawi ya YANGA kugombana kuhusi kuondoka kwa makamu mwenyekiti MOSHA kuwa matawi hayana mamalaka ya kujadili suala la makamu kwani kamati ya utendaji ndiyo yenye uwezo wa kukaa na kujadili hatma ya MOSHA ambaye amejuhudhuru kuongoza klabu ya YANGA ,hivyo kamati itakaa jumatano na itatoa maamuzi ya kamati hiyo kuhusiana na maamuzi ya MOSHA ya kujihudhuru
0 maoni:
Post a Comment