Monday, June 27, 2011

KOCHA MKWASA AKATA TAMAA KUFANYA VIZURI MASHINDANO YA COSAFA

                                  Kocha wa timu ya wanawake MKWASA akiwa anahojiwa na TBC
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanawake CHARLES BONIFACE MKWASA amewataka watanzania wasiwe na matarajio makubwa katika ushiriki wa timu hiyo katika michuano ya COSAFA,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.

MKWASA amesema anahofia timu hiyo kufanya vizuri kutokana na kuwa na muda mfupi wa maandalizi na ukosefu wa mechi za majaribio
Jumla ya wachezaji KUMI na SABA wameripoti katika kambi ya timu ya taifa ya wanawake TWIGA STARS inayojiandaa katika michuano ya COSAFA inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.
Aidha MKWASA amesema kwa sasa anasubiri wachezaji wake muhimu ambao bado hawajapata ruhusa kutoka kwa mwajiri wao ambaye ni JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Michuano ya COSAFA ambayo inajumuisha nchi za kusini mwa AFRICA inatarajia kuanza kutimua vumbi JULAI 2, Mwaka huu nchini ZIMBABWE ikishirikisha nchi za AFRIKA YA KUSINI, MSUMBIJI, BOTSWANA , SWAZILAND, TANZANIA, NAMIBIA, ZAMBIA ,MALAWI pamoja na LESOTHO.

TANZANIA imepangwa katika kundi B ikiwa na timu za BOTSWANA,ZAMBIA na AFRIKA ya KUSINI.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU