Timu ya ZANZIBAR OCEAN VIEW imeendelea kutesa katika kundi lake baada ya kuifunga timu ya READ SEA ya ERITREA kwa bao mbili kwa bila katika mchezo uliofanyika uwanja wa TAIFA Jijini DSM.
Kwa matokeo hayo ZANZIBAR imefikisha pointi sita katika michuano hiyo,lakini kabla ya mchezo katibu mkuu wa timu hiyo alisema klabu ya ZANZIBAR OCEAN VIEW imedhamiria kuleta mapinduzi makubwa katika soka la ZANZIBAR kupitia ushiriki wake katika michuano ya KAGAME CASTLE CUP inayoendelea jijini DSM na MOROGORO.
Katibu mkuu wa OCEAN VIEW, HASHIM SALUM amesema lengo lao kubwa ni kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hii huku wakiangazia wachezaji wapya wa kusajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya ZANZIBAR
HASHIM amewataka wapenzi wa soka wa TANZANIA BARA na wale wa visiwani kuendelea kuziunga mkono timu wenyeji ili kombe hilo libaki hapa nchini.
OCEAN VIEW iko kundi Kundi A pamoja na timu za Simba, Vital‘O ya Burundi na Etincelles ya Rwanda





0 maoni:
Post a Comment