Wasani wa FIVE STAR wakiwa mazoezini kujiandaa na onyesho
Baada ya wanamuziki wake KUMI na TATU kufariki dunia kwa ajali ya gari Mwezi MAY mwaka huu, Bendi ya muziki wa Taarab ya FIVE STARS inatarajia kujitambulisha upya kwa mashabiki wake.
Meneja wa kundi hilo ALI JUMA amesema mbali ya kutambulisha wanamuziki wake wapya , FIVE STARS itapiga vibao vyake vipya kwa mara ya kwanza onyesho litakalofanyika katika ukumbi wa TRAVERTINE, MAGOMENI jijini DARE ES SALAAM.
Miongoni mwa vibao vitakavyotambulishwa ni MWENYE HILA HABEBEKI, SINA GUBU NINA SABABU.





0 maoni:
Post a Comment