Monday, July 18, 2011

MASHINDANO YA VIJANA KUANZA KESHO


 Makocha wa timu za Taifa kushoto KING PAULSEN na JAN PAULSEN pamoja mkurugenzi wa ufundi SUNDAY KAYUNI
Mmoja wa wafanyakazi wa AIRTE; akikabidhi jezi wa mwalimu wa sekondari ishala ya kuanza kwa mashindano ya wanafunzi wa sekondari.

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF)limefanya droo ya mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayofahamika kama AIRTEL RISING STARS ambayo yanaanza kesho jijini DAR ES SALAAM.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema jumla ya sekondari ISHIRINI na NNE zitashiriki katika michuano hiyo kutoka katika mikoa ya DARE ES SALAAM, MOROGORO, IRINGA na MWANZA.

Viwanja vitakavyotumika ni pamoja a MAKONGO SEKONDARI, JITEGEMEE SEKONDARI, TEMEKE na UWANJA WA KUMBUKUMBU YA KARUME.

Mechi za AIRTEL RISING STARS ngazi ya mkoa zitaanza kutimua vumbi mjni MOROGORO, keshokutwa katika uwanja wa MOROGORO SEKONDARI, Ilhali michuano hiyo ikiendelea mkoani IRINGA siku ya JUMAPILI.
Fainali ya michuano hii kitaifa itaanza Mwezi SEPTEMBER, jijini DAR ES SALAAM zikifuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa kwa nchi zinazoongea KIINGEREZA ambayo itafanyika TANZANIA na kusimamiwa na makocha mahiri kutoka katika klabu ya MANCHESTER UNITED.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU