BAADA ya safari za kibiashara huko Ujerumani, msanii wa kizazi kipya, Hamis Chambuso ‘Chief Chamelionair’, amerejea nchini na nguvu ya yake baada ya kuanza kuandaa albamu mpya.
Msanii huyo ambaye alikuwa katika kundi la ‘Fagio la Chuma’, alisema juzi jijini Dar es Salaam kwa sasa anafanya kazi kama msanii binafsi na tayari ameangusha wimbo wa Kilangakomo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, msanii huyo alisema kwamba kibao hicho alichofanya katika studio za Metro, chini ya mtayarishaji Allan Mapigo, kinazeleza kukwama kwa mtu anayejifanya mjanja.
“Kibao hiki kinasikika kila kona, ni kwamba kinaelezea zaidi binti aliyejifanya mjanja kwa kukataa shule na mwishowe maisha yake yanabaki ya kutangatanga kwa kujiuza na kufanya uhalifu,” anasema Chief Chamelionair.
Chief Chamelionair alisema kutolewa kwa kibao hicho ni mwanzo wa kazi nyingine na kwamba albamu yake itakuwa na nyimbo saba kati ya hizo, tano atazifanyia Metro.
Alizitaja nyimbo nyingine ni pamoja na Uhasama, Siku Gani, Mila Potofu, Ili Tuwaweze: “Sina mdhamini. Sina meneja, ila kama tatokea basi itabidi akubali kufanya kazi kwa masharti yangu mimi. Yaani ninavyotaka mimi.”





0 maoni:
Post a Comment