Friday, July 1, 2011

TWIGA STARS YAFIKA SALAMA ZIMBABWE

Twiga Stars imewasili salama hapa Harare leo mchana kwa ajili ya michuano ya wanawake ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) ambapo imefikia hoteli ya Tower Rainbow. Itacheza mechi yake ya kwanza kesho saa 9.15 kwa saa za hapa dhidi ya Botswana.
Mchezo huo wa kundi B utafanyika kwenye Uwanja wa Gwanzura. Timu ilifanya mazoezi leo saa 9 kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo. Wachezaji ambao wanatarajia kuanza kwenye mechi ya kesho kwa mujibu wa Kocha Charles Boniface ni; Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fulkaria Charaji, Mwanaidi Tamba, Sophia Mwasikili (nahodha), Fatuma Bashiri, Mwanahamisi Omari, Eto Mlenzi, Asha Rashid, Fatuma Mustafa na Fadhila Omari.
Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili keshokutwa (Julai 3 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo dhidi ya Zambia kuanzia saa 6.30 mchana kwa saa za hapa. Mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Afrika Kusini 'Banyana Banyana' ambayo itachezwa Julai 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa

6.30.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU