Na Andrew Chale
MSANII anayeng'ara kwenye chati za filamu mbalimbali za Bongo, nchini Tanzania, Elizabeth Michael 'Lulu', ama ‘Hotlulu’ amewaacha maswali magumu ‘friendz zake baada ya kuweka/kupost status ya ‘Bado nipo nipo sanaaaa’. kwenye kurasa ya facebook yake.
Hotlulu ambaye kwa sasa anakula sahani moja na mastaa nyota wa bongo ameendelea kuwaashia endiketa hasa kutokana na uzuri wake aliyo nao huku akipambana na changamoto mbalimbali zikiwemo ‘skendal’ ambazo mara zote amekuwa akizikana.
..Hata hivyo kwa kile ambacho amegonga vichwa na status yake hiyo, ni hali ya huko nyuma kwa nyota huyo kudaiwa kuvishwa pete na jamaa (chini ya kapeti) huku pia akidai kuwa angejitoa facebook, wengi walidhani hivyo viwili lakini Lulu aliwapotezea huku swala la kujitoa alidai kuwa alikuwa anatingisha kiberiti kama kimejaa??/.
….Lulu ndie msanii pekee aliyeanza sanaa toka akiwa na umri mdogo kwenye kundi lililovum Bongo la Kaole sanaa group, ambalo kwa sasa ndilo kundi pekee lililozalisha mastaa wa bongo, akiwemo Ray Kigosi na Steven Kanumba.





0 maoni:
Post a Comment