Monday, July 11, 2011

SERIKALI YAUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA KUKATIKA KWA UMEME

 Serikali imehuzunishwa na tukio la jana la kukatika kwa umeme wakati wa mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la KAGAME kati ya SIMBA na YANGA mchezo uliofanyika uwanja wa TAIFA Jijini DSM.

Taarifa hiyo imetolewa na katibu mkuu wa Wizara ya habari Vijana,utamaduni na michezo kuwa tukio hilo halikutazamiwa hivyo serikali inaahidi wananchi hususani wapenda michezo kwamba tukio kama hilo halitatokea tena .

Kwa kutambua uzito wa suala hilo Wizara ya habari vijana utamaduni na michezo imeunda kamati ya watu wane kuchunguza sababu zilizosababisha umeme kukatika,kamati hiyo itaongozwa na Naibu katibu mkuu wa Bi SIHABA NKINGA.

Kamati hiyo inatakiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya siku saba kuanzia Jualai 12 na itakabidhi taarifa yake kwa waziri wa habari vijana utamaduni na michezo EMMANUELI NCHIMBI.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU