Tuesday, July 12, 2011

WACHEZAJI WA RED SEA WATATU WAJISALIMISHA

 
SERIKALI inawafanyia mahojiano wachezaji KUMI na TATU wa timu ya RED SEA ya ERITREA ambao wamejisalimisha wizara ya mambo ya ndani ya nchi mwishoni mwa wiki iliyopita kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Wachezaji hawa ambao walikuwa katika michezo ya kombe la KAGAME ambayo yalimalizika jumapili iliyopita walikuwa wamepangiwa kuondoka nchini tarehe TISA mwezi huu kwa ndege ya shirika la ndege la KENYA kurudi kwao lakini hawakuonekana uwanja wa ndege kwaajili ya safari hiyo.

MSEMAJI wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi , ISAAC NANTANGA amesema mahojiano haya yanafanywa na idara ya wakimbizi ambayo pia ni utaratibu unaotekelezwa kufuatana na sheria za nchi na za kimataifa kuhusu watu wanaoomba hifadhi, pia mahojiano haya yanafanywa ili kujua sababu zilizowafanya wachezaji hao kutotaka kurejea kwao ni sababu zinazoweza kuwapa sifa ya kupewa hadi ya ukimbizi kufuatana na sheria za kitaifa na kimataifa.

Wakati wakiwa hapa nchini wachezaji hao wanahifadhiwa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na pasi zao zinashikiliwa na idara ya uhamiaji.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU