Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kufunga michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Sherehe za ufungaji wa mashindano hayo yaliyoshirikisha mataifa 10 wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na timu mbili mwalikwa zitafanyika Desemba 10 mwaka huu baada ya mchezo wa fainali utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
JAMA MBA AOMBEWA ITC CAMEROON
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Robert Jama Mba ambaye ni raia wa Cameroon ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili acheze soka nchini humo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetuma maombi hayo jana (Desemba 5 mwaka huu) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kupata hati hiyo.
Mba ambaye aliichezea Yanga enzi za uongozi wa Imani Madega ameombewa ITC kwa ajili ya kujiunga na klabu yake ya zamani ya Tiko United baada ya mkataba wake ndani ya Yanga kumalizika.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na ITC itatolewa wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika.
MAKOCHA 40 KUWANIA LESENI B CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha majina ya makocha 40 wa Tanzania kushiriki katika kozi ya ukocha ya leseni B ya shirikisho hilo. Makocha wote waliopitishwa wana cheti cha ukocha cha ngazi pevu (advance).
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ni miongoni mwa makocha hao watakaoshiriki kozi hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 19-22 mwaka huu.
Wengine na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa (Dar es Salaam), Michael Bundala (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), John Simkoko (Morogoro), Juma Mwambusi (Mbeya), Samson Mkisi (Mbeya) na Sylvester Marsh (Mwanza).
Salum Madadi (Dar es Salaam), Mohamed Nyange (Dodoma), Madaraka Bendera (Arusha), Ally Mtumwa (Arusha), Charles Mkwasa (Dar es Salaam), Idd Mshangama (Dar es Salaam), Hassan Mlwilo (Dar es Salaam), Mohamed Msomali (Morogoro), Mbarouk Nyenga (Tanga) na Leopard Mukebezi (Dar es Salaam).
Mohamed Tall (Dar es Salaam), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam), Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Oscar Korosso (Mbeya), Charles Kilinda (Pwani), Fred Minziro (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Kagera), Hamimi Mawazo (Mtwara), Rogasian Kaijage (Kagera), Eugene Mwasamaki (Dar es Salaam) na Mohamed Mozi (Tabora).
Charles Matoke (Dar es Salaam), Peter Magomba (Singida), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Juma Nsanya (Tabora), Jamhuri Kihwelo (Dar es Salaam), Gilbert Mahinya (Tabora), Juma Mzigila (Morogoro), Joseph Sehaba (Dodoma), Charles Mngodo (Dodoma) na Mohamed Rishard (Dar es Salaam
0 maoni:
Post a Comment