Monday, December 5, 2011

ZANZIBAR HEROES OUT

Timu ya ZANZIBAR HEROES imetupwa nje ya michuano ya  CECAFA TUSKER CHALLENGE baada ya kuambulia kipigo cha magoli mawili kwa moja dhidi ya timu ya RWANDA katika mchezo ulifanyika uwanja wa Taifa Jijini DSM.

 Katika mchezo huo uliokuwa  mkali timu ya RWANDA imeweza kuitoa nje ZANZIBAR HEROES kufuatia bao la pili lililofungwa na mshambuliaji wake KAGERE MEDY kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na OLIVIER KAREKEZI

RWANDA ndio ilikuwa ya kwanza kupachika bao kupitiakwa JEAN BAPTISTE MUGIRANEZA wakati bao la ZANZIBAR likifungwa na ABDULRAHMAN MOHAMED katika dakika ya kwanza ya kipindi cha PILI.

Katika mchezo wa r obo fainali ya kwanza SUDAN imeweza kutinga katika hatua ya NUSU FAINALI baada ya kuilaza BURUNDI kwa Jumla ya MABAO MAWILI kwa BILA.
Kwa matokeo hayo timu za RWANDA na SUDAN zitakutana katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa siku ya ALHAMIS.

Hapo kesho kutakuwa na michezo mingine miwili ya ROBO FAINALI ambapo katika mchezo wa Mwanzo UGANDA itachuana na ZIMBABWE  ambayo itaonyeshwa na TBC 2,Ilhali wenyeji TANZANIA BARA ama KILIMANJARO STARS wakipambana na MALAWI katika mchezo wa pili utakaorushwa moja kwa moja na TBC

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU