Monday, December 5, 2011

NBC FAMILY DAY

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto)
akishiriki kusakata dansi lililokuwa likiporomoshwa na bendi ya FM
Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia
wa benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana
katika mbio za magunia katika Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika
Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam jana. Robert  Kusekwa (wa pili
kulia) alibuka kidedea.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana
katika kuvuta kamba ili kumpata mshindi  katika Siku ya wanafamilia ya
benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana
katika mchezo wa kufukuza kuku katika Siku ya Wanafamilia ya benki
hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.  Mshindi wa mbio
hizo huondoka na kuku huyo na kwenda nae kumfanya kitoweo au kumfuga.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC wakifurahi katika
bwawa la kuogelea ikiwa ni baadhi ya burudani kuadhimisha Siku ya
Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Ofisa Uhusiano wa NBC, Eddie Mhina akigawa zawadi kwa baadhi ya
watoto wa wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa sherehe za Siku ya
Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU