2012. Semina ya Mawakala watakao andaa mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2012, itafanyika tarehe 29 na 30 Machi 2012 katika Hotel ya Giraffe iliyopo eneo la Kunduchi jijini D’salaam.Semina hii itawahusu Mawakala wa Mikoa, Kanda na Elimu ya Juu tu.Baada ya Semina hii Mawakala wa Mikoa wataendesha semina kwa Mawakala wa Wilaya katika Mikoa husika..
Hii itakuwa semina elekezi ambpo pamoja na mambo mengine Mawakala watakumbushwa Kanuni, Sheria na Taratibu zinazoendesha mashindano ya Miss Tanzania. Semina pia itajadili changamoto mbalimbali za shughuli za Miss Tanzania na pia kuweka mikakati ya kupata washiriki wenye sifa na kujifunza masuala ya Udhamini.
Orodha ya Mawakala watakao andaa Mashindano ya Urembo ya Redds Miss Tanznaia 2012 imeorodheshwa. Katika kiambatishi b na c Mashindanbo ya Redds Miss Tanzania kwa mwaka huu yanadhaminiwa na kampuni ya TBL Kupitia kinywaji chake cha Redds Original na yanafahamika kwa jina la Redds Miss Tanzania.
0 maoni:
Post a Comment