Saturday, March 10, 2012

YANGA CHALI KWA AZAM

 Vijana wawili wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi, wakizaniwa kuharibu viti na kusababisha vurugu uwanjani hapo.
 Mwamuzi wa mchezo huo, Israel Mongo, akitoka baruti 'Nduki' kuwakimbia wachezaji wa Yanga baada ya kutoa kadi mbili kwa wachezaji wa Yanga, jambo ambalo lilipingwa na wachezaji wa Yanga na kuzua mtafaruku uwanjani hapo.

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ambapo timu ya AZAM FC imefanikiwa kuketi katika kilele cha ligi hiyo baada ya kuicharaza Yanga magoli MATATU kwa MOJA katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini DSM.

Katika mchezo huo Mwamuzi wa mchezo huo ISRAEL NKONGO alipigwa na mmoja wa wachezaji wa YANGA na baada ya kumzawadia kati nyekundu mchezaji  HARUNA NIYONZIMA kipindi cha kwanza cha mchezo.

Kadi hiyo ya NYONZIMA ilileta kizazaaa kwa wachezaji wa YANGA na kufanya mchezo huo usimame kwa muda wa dakika KUMI.

Katika mchezo  huo YANGA walicheza pungufu baada ya mwamuzi huyo kuumpa kadi nyekundu mchezaji mwingine wa Yanga NADIR HAROUB CANAVARO akidhani kipigo alichopata kilitoka kwa mchezaji huyo      

AZAM walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 4 kupitia kwa mchezaji JOHN BOKO ,NA bao la pili likafungwa na mchezaji KIPRE BALOUU na bao la tatu likafungwa na mchezaji yuleyule JOHNBOKO.
Yanga walipata bao la kufutia machozi kutoka kwa mchezaji HAMIS KIIZA.
Nje ya uwanja mabomu ya machozi yalitawala  baada ya askari kuwatawanya baadhi ya mashabiki kwa kutumia mabomu ya machozi.

Kwa matokeo hayo timu ya AZAM imepaa hadi juu ya msimamo wa ligi kuu TANZANIA BARA kwa kufikisha pointi 41 ,ikifuatiwa na SIMBA yenye pointi 40 na YANGA ikiwa na pointi zilezile 37.
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU