Monday, July 23, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE YA SEKONDARI MTIPA ILIYOPO MKOANI SINGIDA

Meneja Huduma kwa Jamii wa Kampuni ya Simu za Mikononi Tanzania ya Airtel, Hawa Bayuni (kushoto) akikabidhi vitabu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwakilishi wa Shule ya Sekondari Mtipa iliyopo mkoani Singida, Bi. Mary Haiki ambaye alitembelea makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi kuu ya Airtel jijini Dar es salaam


Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.


Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni. Shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milioni mbili.

Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia,Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salaam Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayuni alisema" Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza Bayuni.

Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika kutimiza malengo tuliojiwekea.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa computer 4 na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini. Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU