Tuesday, July 31, 2012

KUPATA HUDUMA YA AIRTEL MONEY SASA PIGA *150*60# BURE

 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa namba fupi *150*60#  itakayotumika kupata orodha (Menu)  ya Airtel money pamoja na kuzindua promosheni inayomuwezesha mteja wa Airtel  kutuma na kupokea pesa bure.  pichani kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde. Uzinduzi wa promosheni na utambulisho wa namba hiyo fupi ulifanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar Es salaam
Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa namba fupi na promosheni ya *150*60#  itakayotumika kupata orodha (Menu)  ya Airtel money pamoja na kuzindua promosheni inayomuwezesha mteja wa Airtel  kutuma na kupokea pesa bure. Uzinduzi wa promosheni na utambulisho wa namba hiyo fupi ulifanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar Es salaam.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa  muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure  

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi  nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma  na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa  na mengine mengi

tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60#   na kuunganishwa moja kwa moja

vilevile  tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha  wateja wetu wote na wakala  wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii  iliyorahisi ni rahisi aliongeza” Mmbando

Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha  na kusaidia wateja wetu kuokoa muda  kwenda mbali kupata huduma za kibenki.

Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU